Tanzania na uongozi mpya

Written by Angela Francis | Posted on  10 Nov.

Watanzania wameamua oktoba 25 mwaka 2015 kumteua kiongozi wamtakaye kwa kupiga kura ili aongoze kwa miaka mitano ijayo. Nikiwa miongoni mwa watanzania takribani milioni 22 nimepata nafasi kwa mara ya kwanza kumchagua kiongozi mpya atakayeshika atamu ya taifa hili. Kuchagua uongozi au utawala mpya wa mwaka huu kwangu unamaana kubwa sana, kwanza nikiwa nauhakika kila maamuzi yatayofanyika kuanzia bungeni hadi kwenye ngazi ya serikali za mtaa inatokana na kura yangu mija katika kuwachagua kuwaweka madarakani Pili utawala mpya kwangu ni mwanzo wa maendeleo ya Tanzania, naamini kila kiongozi anawajibu kulitumikia Taifa lake katika kuleta maendeleo, hususani katika mwaka huu ambao ushindani ni mkubwa si kwa chama tawala tu bali hata kwa upinani, kwani kunavyama vipya vinavyotoa changamoto katika upinzani. Tatu kwa chama chochote kitakachoshinda mwaka huu kinawajibu mkubwa wakuwaridhisha watanzania wengi wenye shauku ya maendeleo na wamabadiliko katkika kila sekta, Kwa kusikiliza na kuangalia sera mbalimbali za vyama naamini uongozi mpya utaleta matumaini ya maisha nafuu kwa mtanzania, kwani elimu ikitolewa bure hasa katika nyanja ya msingi, na ulipaji wa kodi ukapungua kwa kiwango kikubwa watanzania walio wengi wataweza kukidhi katika vipato vyao vidogo watakavyokuwa wanapata. Kwa asilimia kubwa wa naamini Tanzania haitakuwa sawa kimtazamo na kifikra, na hata kujitoleo na kijituma mwaka huu kwani vijana ambao ni zaidi ya silimia 50 wameamka na wako kimtazamo wakizalendo zaidi, kulitetea taifa lao na kama utawala ujao utawatumia vizuri vijana nauhakika Tanzania ya kuanzia mwaka huu itakuwa tofauti na miaka iliyopita.