Siku ya uchaguzi

Written by Lyen Charles | Posted on  2 Nov.

Ni alfajiri na mapema naamka nina furaha sana. Ile ndoto niliyokuwa ninaiota kwa muda sasa imetimia. Kiu niliyokuwa nayo inapata maji, njaa niliyoisikia leo inapata chakula. Oktoba 25 2015 ni siku niliyoisubiri kwa hamu na sasa imefika. Natoka nyumbani nimejiandaa vilivyo, mkononi nimeshika kikatio changu kwa ajili yakumkata yule nisiye muhitaji. Kwa miezi kadhaa nimekuwa nikisikiliza sera za wagombea na kuhoji ufanisi wa ahadi zao. Tayari nimeshaamua kiongozi ninaye muhitaji na sasa nimefika kituo cha mpiga kura kufanya lililonileta.  Ghafla nakutana na foleni ndefu nisiyoitegemea, nikajiunga nakusubiri. Jua kali lilinichoma, jasho lilinitoka nikakata tamaa maana foleni inakwenda taratibu. Moyoni nikajiulizae kipi bora, shida ya masaa machache au shida ya miaka 5? Sekunde, dakika, lisaa na masaa yalipita na ilipofika saa nane mchana nikapiga kura. Nilifurahi sana, nilishangilia na nilijisikia wathamani. Kupiga kura ni haki yangu na mimi nimetimiza wajibu huu kwa kuwachagua viongozi ninao waamini. Mimi Lydia Charles moyo nimeshiriki kikamilifu nakuamua hatma ya maendeleo ya nchi yangu kwa kushirikiana na vijana wenzangu.