Kujitokeza kwa vijana kwa kiasi kikubwa.

Written by Radhia Malla | Posted on  24th Dec 2015.Kujitokeza kwa vijana kwa kiasi kikubwa, kwenye michakato yote Kipindi cha uchaguzi na kujitokeza Kupiga kura mwaka huu, kumenipatia mtazamo tofauti na mkubwa sana,kwanza kuwa na uwezo wa kuuzungumzia kuwa ulikuwa na utofauti mkubwa sana ,kwakuwa kulikuwa na muamko mkubwa sana wa kisiasa hasa kwa vijana, kwakuwa idadi kubwa ya vijana ilikuwa ni mala yetu ya kwanza Kupiga kura, hivyo kupelekea 56% ya vijana Kupiga kura. Mtazamo wangu juu ya sura ya uongozi na utawala mpya baada ya uchaguzi, ni kuona majibu ya changamoto zilizokuwa, zikitafutiwa ufumbuzi kwa takribani miaka yote kwa ajili ya vizazi vijavyo pia.

kwakiasi kikubwa uongozi huu umekuwa ni wautofauti sana, kwakuwa umekuja na majibu na njia nyingi hasa za kuwasaidia vijana kwenye swala zima la ajira, na hata kuwa na mipango kazi mikubwa ya kukuza uchumi wa nchi kwa kudhibiti na kupambana na rushwa,pia hata kutengua na kuondoa uongozi mbovu kwenye wizara husika. Jambo ambalo limeleta matumaini makubwa, kwakuwa kwa kiasi kikubwa watanzania tulikuwa na kiu ya kutaka kujua, utendaji wa serikali kwa vitendo na sio maneno. kunamatumaini makubwa sana dhidi ya serikali ya awamu hii ya tano, kwakuwa kunaviashili vikubwa vya kuonyesha kukuza uchumi.

Ikiwa ni kama mwezi kuisha tangu Mh. John Pombe Magufuli kuanza kazi ,kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa mdamchache kama vile, kuhakikisha hospital zote zinakuwa na vitanda vya kutosha. Kazi nzuri inazidi kufanyika kwa kuambatana vema na waziri mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, kwa kuudhihilishia umma wa watanzania kwa kufufua na kuweka wazi, madudu yaliyokuwa yanarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kutaka kudidimiza uchumi. Pongezi kwa uongozi wa serikali ya awamu hii ya tano, hakika kwa kushirikiana na wananchi tutapeleka taifa mbali na kuleta maendelo, bila kuangalia udini, ukabila wala uchama.