Nimeshiriki

Written by Nickson George | Posted on  2- 12-2015.

Kama kijana wa kitanzania nimeshiriki kwenye Uchaguzi huu wa mwaka huu kwa njia kubwa tatu tofauti. Kwanza nilianza kushiriki kwa kuchukua jukumu la kuhamasisha watanzania  na vijana wenzangu kupitia mitandao  ya Kijamii kuwahamsisha kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura na kudumisha amani kama vijana wazalendo na wenye mapenzi ya dhati na nchi na hili nililifanya kwa kubuni hashtag kama #pigakurakwaamani na hata kutumia #KuraYetu  kufanya kama trend ambayo imehamisisha vijana wengi ambao waliipost na kushawishi vijana wengi kuweza kupiga kura. Njia ya pili nimetumia vipindi vya Radio na Tv ambao niliproduce na hata kutangaza kutoa elimu ya umuhimu wa kupiga kura kwa hasa kwa sisi vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa. Njia ya tatu nimeshiriki moja kwa moja kupiga kura kutimiza haki yangu ya kikatiba ya kupiga Kura na kuwachagua viongozi kuanzia ngazi ya mtaa ,kata, jimbo na hata taifa siku ya tarehe 25 October2015  huku nikizidi kuhamasisha vijana na wananchi wengine kuzidi kutunza amani kwa maendeo ya taifa ambalo liko chini ya uongozi mpya... Kama kijana ambae nilipiga kura kwaajili ya uongozi mpya ambao utaongoza nchi yetu nikiamini utaleta maendeleo makubwa ,nimejitoa kwa nguvu na hali kushiriki katika kuleta maendeleo makubwa hasa kwa vijana wote wa Tanzania, kwa kufanya kazi kwa bidii, kupitia njia mbali mbali za mitandao, vipindi vya radio na tv na hata kushiriki kwa Vitendo kuhamasisha vijana kufanya kazi kwa juhudi na kujituma kwa bidii ili tuweze kuleta maendeleo binafsi na kwa taifa letu kwa ujumla lakini pia kulipa Kodi na hata kuhamasisha ulipaji kodi zote kwa maendeleo ya ukuaji wa uchumi na maendeleo kasi lakini pia nitashiriki katika mikutano na semina zote za kiserikali zenye kutuunganisha vijana kimaendeleo. Mimi nasema, hapa ni vitendo katika kuleta maendeleo yangu na yetu vijana na taifa kwa ujumla.