Tanzania kisiwa cha amani

Written by Mujuni Baitani | Posted on  2- 12-2015.

Maisha ya binadamu huwa na wakati, muda na nyakati. Yale masaa, dakika na sekunde zilizokuwa zinahesabiwa na watanzania wengi zilitimia kwa muda mfupi tu baada ya kupiga Kura kuchagua viongozi watakao tumikia taifa kwa miaka mingine mitano kama iliyo desturi kwa nchi zenye utawala wa kidemokrasia. Binafsi mwaka huu sio mara yangu ya kwanza kupiga kura ila ni mara yangu ya kwanza kuona maandalizi makubwa yaliyoambatana na mabadiliko ya mifumo ya kupiga kura pamoja na kutoa vitambulisho vipya, pia kumekuwa na hamasa kubwa toka kwa watanzania wengi kujitokeza kupiga Kura kutimiza haki yao ya Kikatiba itokanayo na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 5. Kutokana na maandalizi ya Tume na mrejesho wa wananchi idadi ya wapiga kura imeongezeka kutoka wapiga kura milioni 10 mwaka 2010 hadi million 22.7 mwaka 2015, pia nilistaajabu sana kuona ustaarabu uliyotukuka kutoka kwa wananchi baada ya Kampeni na kwenda kupiga kura kwa ustaarabu na kwa kufata uratibu ulikuwa umewekwa na Tume Ya Uchaguzi nchini ili kutopoteza haki yao ya msingi. Hakika Uchaguzi mkuu wa 2015 Tanzania ulikuwa wa aina yake, makundi maalum yalipewa kipaombele katika kila kituo cha kupiga Kura. Ni hatua kubwa sana kwa taifa letu kuwa na uchaguzi wa Amani na wananchi kuwa na hamasa,sasa tunafurahia tuna Rais mtiifu na mnyenyekevu anatambua shida za Watanzania. Hongera Tanzania kuwa kisiwa cha Amani Mungu ibariki Tanzania