Tathmini ya uchaguzi kwangu

Written by Hassan Pukey | Posted on  2- 12-2015.

Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kazi nzuri walioifanya katika kipindi chote cha uchaguzi (Wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na wakati wa kuhesabu kura mapaka kutangaza matokeo). Pia nitoe pongezi kwa wagombea walioshinda na walioshindwa katika nafasi mbalimbali za uongozi tukianzia na kata, wilaya na nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pongezi kubwa kabisa ziende kwa wananchi ambao walikuwa sehemu kubwa ya kutunza Amani iliyopo hivi sasa, japo kulikuwa na changamoto ndogondogo za kibinadamu. Kiujumla naweza sema uchaguzi ulikuwa huru na haki, kwasababu hapakuwa na mtu aliyeshikiwa bunduki wala panga ili amcahgue mgombea Fulani. Pia hapakuwa na furugu zozote zilizowafanya wananchi washindwe kupiga kura kwa usalama, taratibu zilifuatwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi nchini. Changamoto ndogondogo zilikuwepo, lakini hazikutowesha amani wala kuvunja taratibu za kisheria kwa wapiga kura. Matangazo yalitangazwa kwa kufuata sheria kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi (NEC), japokuwa kuna baadhi ya wagombea walikiuka sheria. Baada ya hayo yote, napenda kusema kwa upande wangu uchaguzi ulikuwa huru na haki. Pia tunashukuru Mungu hapakuwa na machafuko yoyote yenye madhara kwa ustawi wa Taifa letu, watanzania tumekomaa kisiasa maana ni jambo kubwa na lakustajabisha kwa Mataifa ya jirani kama Kenya, Uganda, Burundi nan chi za magharibi. #TanzaniaBora #UhuruNaKazi #TaifaKwanza