UTAWALA BORA NI SISI…..!!!

Written by Radhia Malla | Posted on  19 Feb 2016.


Vijana wa kitanzania ni nusu ya jumla ya watanzania wote nchini lakini kuna changamoto kubwa sana kwetu vijana, hasa linapokuja swala zima la serikali na utawala bora. Vijana wengi tunaamini kuwa ni jukumu la serikali kututekelezea kila mahitaji yetu, lakini tunasahau kuwa sisi vijana ndio tuna jukumu la kujenga nchi yetu. Na hii inasababishwa na ile hali ya vijana kukosa majukwaa ya kupatiwa elimu kuhusu serikali na utawala bora, kwa njia ambazo ni rahisi sana kuzielewa. Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya vijana waliopiga kura mwaka 2015, imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana na kufikia 67% ukilinganisha na ile ya mwaka 2010.

Mbali na kuwa vijana wengi ilikuwa mara ya kwanza kupiga kura, lakini majukwaa mbalimbali yanayowahusu vijana hayakuwa nyuma kuelimisha vijana kuhusu serikali na utawara bora. Tanzania Bora Initiative (TBI), ni moja kati ya mashirika yasiyo la kiserikali ambalo liko mstari wa mbele kuelimisha vijana kuhusu mambo mbalimbali, hususani serikali na utawala bora. Kwa kutumia Sanaa na habari kwa kutengeneza majukwaa yahusuyo vijana, ni rahisi kwa vijana kuona umuhimu wao kwa nchi na kutekeleza majuku ya kujenga taifa. Kwa kuona umuhimu na kujua majukumu yetu kama vijana, tuungane na Mh. John Pombe Magufuli ili kuleta maendeleo kwa taifa, kwa kutekeleza msemo “HAPA KAZI TU”.