NASTAHILI KUTHAMINIWA

Written by Angela Francis | Posted on  26th Feb 2016.Huu ni muda sasa wakutambua thamani yangu, hakika ni sawa kabisa na wewe! Nikitazama sioni utofauti wetu, ni kipi kitutie dosari utu wetu na hata kutuwinda hivyo?. Naamini kila mtu yuko huru na watu wote ni sawa kisheria, hata katiba mama inaadhihirisha hivyo,kifungu cha 12 ibara ndogo ya 1 na ya 2 inasema Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthamanini utu wake. Hivyo basi kunamaana kubwa yakuitwa Binadamu wote ni sawa, haijalishi ngozi yangu kuwa utofauti na wewe inanifanya mimi sio mtu. Naamani tukimkitazama mtu zaidi ya maumbile yake ya ngozi hatuna utofauti wowote. Nastahili heshima yangu kama binadamu wenzangu, msinikate viungo vyangu, kwa manufaa ya wenzangu.

Mimi ni kijana mdogo namalengo na mipango mingi yakufanikisha maisha yangu. Ninasoma kwa bidii, natii sheria za nchi na kushirikiana na watu wanaonizunguka vizuri tu, kwa sasa nafurahia maisha yangu yakujifunza, nafurahia nimepata nafasi yakuonesha thamani yangu zaidi ya muonekanio wangu, ninacheza mpira wa michangani lakini naamini kuna siku nitaichea timu ya taifa. Utofauti wetu utufanye kuwa uimara wetu.