Tanzania Na Demokrasia Bora Niitakayo

Written by Basil Komu | Posted on  11 Mar 2016.

Kwa mtu wa kawaida sana akisikia neno siasa atapata wazo la vyama au chama flani katika eneo alilopo, Na katika nchi yoyote iliyokua chini ya ukoloni au udikteta watu wake wakisikia neno Demokrasia huwa wanapata ahueni kwamba sasa maisha yanaanza kua bora kwakua wanaweza kusema lolote ilimradi isiwe kumtusi mwenziwe. Swali la kujiuliza ni Je? huo ndio ukweli wa neno demokrasia katika eneo lile? Je? Siasa ni kuhusu chama? Maana ufahamu wangu ulio mdogo sana unanishawishi kuamini kua siasa si chama wala vyama, na democrasia haimaanishi umekua huru kusema lolote ispokua tuu, kwa zile nchi zinazoelewa maana halisi ya siasa na democrasia.

Naipenda sana nchi yangu ya TANZANIA na ukweli kwamba vijana wengi wamepata ufahamu wa siasa pamoja na demokrasia, basi roho yangu imesuuziiiiiika haswa! Tumepata madiwani vijana, wabunge vijana(NASARI,HALIMA,MBONI,PROF JAY,SUGU, na  waziri vijana na hata baadhi ya wakurugenzi Kama kaka yangu MCHECHU(NHC) nimewataja wachache tuu.

Tatizo au wasi wasi wangu mkubwa kwa watanzania wote wanaoingia na waliokwisha ingia katika siasa ni kwamba; Kwanini tunakosa uelewa wa utofauti kati ya SIASA na DEMOKRASIA? nasema haya kwakua wengi wanakosa uelewa wa kikomo cha demokrasia.

Kubwa ninalokusudia kufikisha kwa wewe unaesoma ujumbe huu sasa ni kwamba; vijana wengi sana tunaingia kwenye siasa za kujifanya kuikomboa Tz kutoka hapa ilipo kuifanya bora zaidi, lakini ukweli ni kwamba tunajidanganya tuu bila mafanikio yoyote. Sababu kubwa ya kusema hivi ni kwamba MWANASIASA yeyote katika dunia ya leo ya siasa na demokrasia anapoweka chama mbele badala ya taifa ujue fika hana nia na nchi au watu bali nia yake ni kukisaidia chama chake dhidi ya chama kingine.

Tanzania ina watu wengi sana hawana vyama kabisa, sasa wewe ukipewa madaraka utawasaidiaje wakati umeweka uchama mbele? Jambo la msingi ni kuweka nchi mbele na maslahi ya nchi yawe kipau mbele katika siasa zako na fikra zako. Nasikitishwa sana ninapoona viongozi wakubwa kabisa wa nchi Mf(Rais,Waziri,Mkurugenzi,Mbunge na hata kiongozi wa dini) Anahutubia au kuzungumza na wananchi kavaa sare ya chama flani, hili ni jambo la aibu na linaonyesha jinsi gani hatujakua kisiasa na katika kuweka mbele maslahi ya Taifa hili.

Sare za vyama zivaliwe wakati wa mikutano ya vyama pamoja na kueneza propaganda za kichama ila si katika mikutano ya kitaifa ambayo inahusu watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama.
SIKITIKO ZITO MOYONI MWANGU ni pale ninapomsikia mtanzania anasema Serikali hii ya CCM imeshindwa kufanya jambo flani, hivi kweli serikali ni ya CCM au ya watanzania? Au ndio tunataka kuibebesha CCM lawama zisizowahusu? Serikali hii ni ya Watanzania na sio CCM wala chama kingine, Tuseme serikali ya Tanzania imeshindwa maana Serikali ni watu na watu ndio sie wote wenye uraia au paspoti ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayomilikiwa na watanzania wote kisheria


MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA MACHO YETU YAFUMBUKE! AMINA