Serikali Yangu!

Written by Basil Komu | Posted on  11 Mar 2016.

 Wakati nikiwa naishi kwa furaha,majivuno ya nchi yangu nzuri yenye utajiri na amani yakutosha na pia kuweza kupambanua mambo ilikua ni mwanzoni mwa miaka ya 80 niliona watu wakiishi kwa ujamaa maana ilikua jambo la kawaida sana kwenda kula au hata kulala kwa jirani bila wasi wasi; na maisha yalikua burudani sana kwakua tulikua tukiombana moto,chumvi,unga,mafuta ya kupikia,ya taa na hata machanuo kwaajili ya kuchana nywele.

 Wakati huu sikuwahi kusikia mtu kaua au kuuwawa na mtanzania mwenzake ila sasa ndio imekua kurasa za mbele za magazeti kama tulivyokua tukiona kutoka kwa nchi za wenzetu,Tulikua tukimwona Baba wa Taifa hili akiwa kavalia kaunda suti na fimbo mkononi na akipita kila kona ya nchi tukiwa tunaimba ule wimbo wa Taaaaanzania tanzaniaaaa nchi yenye ....... na ikifika saa12jioni kila mtu anatii amri ya kushusha bembera yetu nzuri.

 Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90 tulikua tukitumie zile noti zetu zenye ubora na picha mbali mbali za mali asili ya Tanzania na tukiwasiliana kwa barua(s.l.p), nilikua nikiona wakubwa zangu wakipendana na kujumuika pamoja kwenye sherehe mbali mbali kama EID,KRISMAS,KOMUNIO NA KIPAIMARA! Na wakati huo ukisikia siasa utamsikia Cleopa Msuya, Agustino Lyatonga Mrema, John Momose Cheyo nk.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 nikiwa Sekondari tukiwa chini ya Mzee wetu Mkapa kiongozi aliekua Imara na mwenye maamuzi magumu na yenye kusimamisha jamii kwenye mstari sahihi, tulianza kuingia rasmi kwenye teknolojia mpaka viganjani.Suala la bara bara ya shauri moyo lilileta mtafaruku kidogo baada wa wanadini kukataa barabara isipite makaburini. Ila kiongozi imara akazungumza na kazi ikafanyika na leo tunafurahia bara bara ile na Machinga complex imejengwa pale.

 Mwishoni mwa miaka ya 2000 tukiwa na MH RAIS J M KIKWETE, Nchi yangu ninayoipenda kwa dhati ikiwa chini ya vyama vingi nikiwa na imani kwamba ndio tunasonga mbele na kuendelea kupeperusha bendera ya Amani na Upendo Duniani, gafla bendera ile ikaanza kwenda kinyume na mwelekeo wa upepo wa Amani yetu. NAKUMBUKA VYEMA MH KAKA YANGU NINAEMWESHIMU SANA ZITTO KABWE alichangia maada ya Wizara ya katiba na sheria kuhusiana na mjadala wa mahakama ya Kadhi hapa tz na akasema, nanukuu "tz ni nchi inayoheshimu dini zote na haifungamani na upande wowote ila wanasiasa wetu wanapandikiza utofauti wa kidini ambao ni sumu kali itakayo angamiza vizazi vyetu'

 Ndugu zangu maneno ya Mh ZItto ni mazito sana na ukiyachambua kifalsafa utapata maana kubwa na kuona kua alikua akilenga mbele na si kwa wakati ule, wakati haya yakisema na mh, kuna wengine walikua wakibeza na kusema wapinzani hawana jipya wanatafuta sympath kutoka kwa wananchi.

 Leo hii naandika maneno haya ni mwanzoni mwa mwaka 2016 nchi yangu ninayoipenda na nitakayokufa nikiitumikia na inayowalea mwanangu ipo katika CHUKI,FITNA NA MAUAJI YA KIDINI ,RANGI ambayo yanahitaji kiongozi mwenye nguvu na uchungu na nchi hii kuyamaliza kwa kutumia fimbo yake ya uongozi na vyombo vya sheria kama alivyofanya mkapa wakati wa Shauri moyo.

 Kiini cha dini yoyote ni  kuimarisha Amani na kueneza utulivu na upendo miongoni mwa waumini wake na si kueneza njia za kulipiza kisasi endapo kuna aliekukosea kwa kua kusamehe ndio misingi ya dini zetu. Malumbano yanayoendelea ya kidini na chuki zitakazoangamiza vizazi vyetu ni yakukomeshwa kwakua bado tuna nanafasi na watanzania ni wasikivu na waelewa sana.

 Niwakati umefika tujue kua hawa wanasiasa na viongozi wa dini wanaochochea vuruga hii leo, vurugu hizo zikianza watakua wakwanza kukimbiza familia zao nje ya nchi na sisi ndio tutakaobaki kuumia na kuuana, kama kuna ambae amefika kwa jirani zetu Kenya,Uganda na Rwanda ataelewa ninachosema. Maadhara ya vurugu za kidini ni kuuana,kuchukiana,kutosaidiana na mbaya zaidi kubaguana kwa itikadi!  Je, tumefikia hatua yakwenda kinyume na maandiko ya vitabu vyetu vya dini?

 Mzee PIUS MSEKWA na SAMWELI SITTA ni viongozi wakujivunia katika nchi hii kwakuliongoza vyema bunge letu bila kujali itikadi za chama walichotoka ila walitambua fika kua wapo katika kiti kwa manufaa ya Taifa hili lililojaa wa…… kama hao wanaoporomosha matusi na mabishano binafsi ndani ya Bunge Tukufu(ingawa naona hata aibu kuliita Bunge Tukufu kwa haya yanayofanyika ndani yake)

 Mama yangu aliwahi kuniambia (BORA MATAPISHI KULIKO UOZO TUMBONI) serikali yangu waachen wananchii waseme au wabwabwaje kama msemavyo kuliko kuwapandikiza chuki miyoyoni mwao.

Kabla ya hitimisho niseme kwamba tuwe sana makini na hizi social media zetu maana ni rahisi sana kusambaza mawazo hasi na asie mwerevu ni rahisi kufuata alichosoma na kukifanyia kazi.

 Ndugu zangu nchi hii haiongozwi na Muislam wala Mkristo bali inaongozwa na mtanzania aliechaguliwa na watanzania wote yaani WAKRISTO,WAPAGANI NA WAISLAM.

 MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WABARIKI VIONGOZI WANGU NA UWAPE WEREVU WAKUWEKA TAIFA MBELE  KATIKA  MAJUKUMU YAO.