KIPAJI CHANGU, MANUFAA YETU..!!

Written by Radhia Malla | Posted on  18 Mar 2016.

Ningumu sana kugundua kuwa kipaji kinathamani sana kwenye jamii, nahii inatokana na kuwa jamii nyingi haiamini kuwa vipaji husababisha mabadiliko chanya. Vipaji vingi hupotea kutokana na kukosa support kwa jamii husika. Kunamanufaa na faida nyingi sana endapo vipaji vikatambulika mapema, na kupewa vipaumbele ili kuleta maendeleo. Tunaona kwa kupitia vipaji tofauti leo Tanzania imeweza kupata sifa mbalimbali. Hivyo basi sio kwenye jamii tu lakini hata nchi kiujumla. Kikubwa ni kujitambua binafsi kipi ni kipaji ili uweze kukifanyia kazi.

Kujiamini na kujituma ni sifa kubwa kwa kiongozi yeyote yule, Ningumu kuishi na kuongoza watu toka mikoa na mataifa tofauti, wenye asili, Imani, lugha, mtazamo, mawazo, na tabia endapo hapatakuwa na kipaji cha uongozi. kujifunza kitu kipya  kila siku kupitia uongozi, najifariji kuona jamii iliyonizunguka ikiniamini kwenye kazi nizifanyazo za kujitoa, na kuwa mstari wa mbele kwa kuwashawishi na kujumuisha vijana wengine kwenye miradi tofauti ya kijamii kimaendeleo. Kujitoa ni nguzo kubwa sana ya mafanikio kwa jamii na pia kuwekeza mda kwenye kazi za kijamii.

 Haikuwa rahisi kufahamu kuwa sauti yangu ni uongozi tosha, kwani kwa kutumia sauti yangu nimeweza fikia hapa nilipo na kuifanya jamii kuniamini zaidi, kwakutumia sauti yangu na kuzungumzia maendeleo na hata kufundisha wengine nilichojifunza na kupelekea utendaji. Naimani kuwa endapo kila kipaji kikipewa kipaumbele kuanzia kwenye familia mpaka jamii itasupport na kukipokea.