MIMI NA MAENDELEO

Written by Qudrah Bernard | Posted on  18 Mar 2016.

Maisha ni safari ndefu ambapo kuna wakati wa furaha, amani  na misukosuko . Ninachoamini ni kwamba kila mtu ana historia yake  katika mafanikio aliyonayo hadi sasa  na inawezekana kwa namna moja au nyingine bado hajaweza kutimiza ndoto zake. Nilipokuwa shule ya msingi nilipenda sana somo la hesabu na ndoto zangu kwa wakati huo zilikuwa ni kuja kuwa  MHASIBU japo pia nilipenda muziki uigizaji  na pia utangazaji  katika runinga lakini sikuipenda kama nilivyopenda uhasibu .Kilichonisukuma zaidi sikupenda kusikia wanawake na wasichana wakinyanyaswa hivyo nikatamani  kuwasaidia.

Nilipofikisha umri wa miaka 14  nilianza kuvutiwa zaidi na kazi ya uandishi wa habari na uigizaji. Ndipo nilipoamua kusomea  maswala ya habari na  ndipo nilipo mpaka sasa.Nilifanikiwa kupata kazi katika kimoja cha radio mwanzoni kabisa nilipoanza chuo, nilipata nafasi ya kuwa mtangazi wa kipindi cha burudani na nilifanikiwa kuwasaidia waimbaji chipukizi, kufikia malengo yao .Na baada ya kumaliza masomo yangu niliweza kupata fursa ya kujiunga na kituo kikubwa cha radio na runinga na hapo niliweza kufanya  vipindi tofauti kama mtayarishaji na baadae  nilijikita kwenye matangazo.

Bado nia yangu  ni kuwasaidia wanawake na wasichana katika mambo mbalimbali tunayokutana nayo kwenye jamii mfano ukatili wa kijinsia , ukeketaji mimba za utotoni nk.Na kwa sasa niko katika kipindi cha Mrembo ambapo kazi yangu kubwa ni kumuelimisha na kumsaidia mtoto wa kike ili aweze kujua na kutambua  haki zake Naamini nitaweza  kuwasaidia wengi kupitia kipaji change na wengi watafanikiwa kupitia mimi.