UMASIKINI WA KUSAIDIANA

Written by Angela Chizumi | Posted on  25 March.

Umasikini umekuwa ni sehemu ya maisha ya watanzania wengi, huku vijana tukilia na ukosefu wa ajira ikiwa ni chanzo kikuu cha umasikini. Swali la msingi tunalo jiuliza nafasi za ajira ziko wapi?.

Huku reporti zikionesha mwaka 1990 nusu ya 1.9 bilion ya umasikini imepungua kwa Millioni 836 kwa  mwaka 2015, lakini bado watu walio wengi wanashindwa kupata mahitaji muhimu hadi hivi sasa.

Umasikini siutazami kwa sura ya mtu asiyeweza kupata mahiyaji muhimu, umasikini kwangu ni kupotea kwa hali yakusaidiana hususani kwa watu wote wenye kipato, namaanisha huhitaji kuwa na mali nyingi ndio uone uhitaji wakumsaidia jirani yako. Msaada unaweza kuwa wakimawazo, wakifikra, kakihali na labda fedha.

Haina maana basi tusema uchumi wa nchi umepanda kwa Tanzania, na tukafurahia huku wenzetu, kaka, dada, baba na mama zetu wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku.

Naamini! Umasikini utaendelea kuwapo ikiwa tu hali yakujalana na kusaidiana itatoweka.