IPI MAANA HALISI YA NJAA?

Written by Radhia Malla | Posted on  1 April, 2016.

Asilimia kubwa ya watu wanaokumbana na tatizo la njaa duniani ,wanaishi kwenye nchi zinazoendelea, ambapo ni Zaidi ya 12.9% ya watu hao hupatwa na utapiamlo. Kinachosikitisha Zaidi ni kuwa, asilimia kubwa ya watu ambao hupoteza maisha kwa tatizo hilo ni watoto. Takribani million 66 ya watoto toka nchi zinazoendelea, huudhuria masomo wakiwa na njaa. Na million 23 kati yao wanatokea bara la afrika.

Kiuharisia kilimo ndio chanzo kikubwa cha kipato na hata ajira duniani. Tangu mwaka 1900’s kilimo kilikuwa kikizalisha 75% ya chakula dunini. Na matazamio ya maendeleo endelevu ni kuwa ifikapo mwaka 2030, njaa isiwepo wala upungufu wa chakula usiwepo. Kwa kukuza na kuongeza uwekezaji kwenye kilimo,sayansi na tecknolojia.

Lakini huwa najiuliza sana hili swali , hivi ni ipi tafsiri sahihi ya neno NJAA? Nikweli kuwa njaa tuizungumziayo ni ile ya kukosa chakula bora pekee? Na vipi kuhusu njaa ya madaraka ambayo hupelekea ukosefu huo wa chakura bora. Inasikitisha sana kuona nchi nyingi zikiendekeza njaa za madalaka na kusababisha njaa ya chakula. Huu ni mda wetu wa kufikiria jinsi gani tutaweza kukuwa, na kugawana chakula tulichonacho. Ili misemo kama hii tusiweze isikia tena , “Tafadhari sijala toka jana naomba nisaidie”, “Asante sana kwa kunipatia hiki, angalau nami nitakula”, “Tutawezaje kufanya shughuri za kimaendeleo ,kama kunavita mpaka sasa?”. Na misemo hii hutokea duniani kote na tunaisikia kila siku