NAHESHIMU MCHANGANYIKO

Written by Eberhard Osward | Posted on  15 April, 2016.

Siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, umoja hapa nazungumzia umoja wa kitaifa na kimataifa. Siku zote huwa naheshimu na ninafurahi kuona watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanafanya kazi kwa umoja. Dunia imeshakuwa kijiji, tumeshakuwa wamoja hivyo sioni sababu ya kuendelea kubaguana kwa dini, kabila na hata utaifa. Sisi sote ni ndugu kama alivyosema Innocent Galionoma  https://youtu.be/MJXmvxqTfNw kwenye nyimbo yake, Innocent ameelezea faida ya kuishi kama family, kama wamoja hivyo basi kama binadamu tunatakiwa kufanya kazi kwa umoja bila kujali mataifa, rangi na hata dini, Hayati Lucky Dube alisema bila kujali tofauti za rangi sisi ni wamoja, angalia link hii kusikiliza maneno yake https://youtu.be/R4csXJXHVGA

Hivyo basi kuanzia sanaa, hadi vitabu vya dini vinaongea kuhusu kuchanganyika na kufanya kazi bila kubaguana, kwanini tutengane, kwanini tusifanye kazi kwa umoja, inapendeza mtu kutoka America kufanya kazi na mtu kutoka Tanzania, mtu kutoka Europe afanye kazi na mtu kutoa Asia, Umoja na Ushirikiano unaleta ubunifu, unaleta amani na upendo.

Umoja na upendo utawale daima.