Mchanga Unajenga Nyumba

Written by Nickson George | Posted on  15 April, 2016.

Tengeneza picha ya kwamba umeamua kuanzisha biashara  flani ambayo either unashirikiana na ndugu zako kadhaa au umeamua kuajiri wafanyakazi  watakao kusaidia kufanya huduma katika  biashara hiyo,lakini  kabla ya kuanza kwa biashara ,ukafikiria kuhitaji misingi ambayo  itasimamia biashara hiyo ambapo ukaona  si jambo baya ukiwashirikisha wafanyakazi wako  nao waseme wanadhani ni misingi  ipi itafaa kuendesha au kutoa huduma ambayo itafanikiwa , na  nguzo hizo ndizo  zitakazo linda  utendaji na ukaaji wa biashara hiyo….mwisho wa siku  kila Mtu akakupa  la kwake  ukapokea kila mchango wa mfanyakazi wako  na kuuamiini kwa moyo mmoja .

Baada ya mwaka mmoja Biashara yako ikakuwa kubwa na kuingiza faida nyingi sana  na siri ya mafanikio ya ukuaji huo  ni jinsi ulivyoamua wewe na wafanyakazi wako  kufanya kazi kwa kufuata misingi  mliyojiwekea  siku ya kwanza  ulipoanzisha Biashara hiyo...

Oiiii please rudisha mawazo ya kutoka kwenye fikra hiyo,lengo la kukupa mfano wa kuwaza hivyo ni  kuonyesha  Umuhimu wa kuheshimu  mchango wa  mawazo ya kila mtu katika ujenzi  jambo ,biashara au ujenzi wa kitu flani…ambapo kwa kizungu wanaita  respect for diversity …ni vipi unaeza heshimu mchango au mawazo ya mtu mmoja  katika ujenzi na mafanikio ya jambo…kwa kifupi kila mchanga unakamilisha ujenzi wa nyumba.