HESHIMA DHIDI YA TOFAUTI ZETU, NDIO MAENDELEO YETU!

Written by Radhia Malla | Posted on  15 April, 2016.

Mara nyingi mambo mengi huwa hayaendi sawa na huchelewa kufanikiwa, kutokana na kutokuheshimiana kwa tofauti tulizonazo. Siri kubwa ya mafanikio ni kuheshimiana kwenye utofauti wa mawazo yetu, kwani utofauti wa mawazo ndio husababisha mafanikio ya jambo. Hata kipindi ambacho nchi zilikuwa zikigombania uhuru, viongozi waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha hayo walikuwa wakiheshimiana kwenye utofauti wao wa fikra na mawazo ili kufanikiwa.

Mashirika, Taasisi,vyama na hata vikundi vingi, vimekuwa vikishindwa kuendelea na hata kufanikiwa kutokana na sabau ya kushindwa kuheshimiana kutokana na tofauti zao. Sio hapo tu lakini pia tukiangalia hata kwenye ngazi za kimataifa pia, kwani kutoheshimiana kutokana na utofauti husababisha madhara makubwa sana. Kwa mfano barani afrika kumekuwa na migogoro mingi sana kwenye baadhi ya nchi, na kupelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe, namaanisha waafrika kwa waafrika jambo ambalo nadhani husababishwa na kutoheshimiana na utofauti baina ya nchi moja na nyingine.

Kubwa la kuzingatia ni kuheshimiana kwenye kila nyanja, ili kuleta maendeleo maana bila heshima hakuna mafanikio wala maendeleo. Utofauti namaanisha umri, kidini, utawala, mamlaka hata kitaifa. Kwani kwenye heshima ndio kwenye maendeleo.