ELIMU NI ZAIDI YA KWENDA SHULE

Written by Eberhard Osward | Posted on  15 April, 2016.

Kuna msemo mmoja wa wahenga unaosema “Elimu ni ufunguo wa maisha”, Pia nakumbuka rais wa kwanza Afrika ya Kusini ambaye pia ni miongoni mwa wanaharakati wa Africa aliwahi kusema kuwa “Education is the most powerful weapon which you can use to change the world.” Akiwa na maana kuwa elimu ni moja kati ya silaha ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuibadilisha dunia,. Leo katika makala yangu nitapenda kuzungumzia elimu, nguvu ya elimu kwa maendeleo ya taifa na jinsi gani katiba yetu ya jamhuri ya muungano imempa kila raia haki ya kupata elimu. Tukianza kwa kuipitia na kuitafakari  ibara ya 11 kifungu cha pili cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inampa kila raia  haki ya kujielimisha, kifungu icho kinasema

11 (2) “Kila mtuanayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake” Kifungu hiki kinatoa haki ya kikatiba kwa raia kuweza kujipatia elimu katika fani anayoipenda kwa lengo kuu la kupanua upeo. Nikija kuutazama uhalisia naona ni sahihi kabisa kuwa elimu ni moja katika nguzo kubwa sana kwa maendeleo ya taifa lolote lakini kwa upande wan chi zetu za kiafrika elimu bado haijafanikiwa kutukomboa, naweza sema maneno haya hasa nikiuangalia mfumo wetu wa elimu ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa wa nadharia, wanafunzi wanasoma bila kujifunza kwa vitendo, hii bado imekuwa na athari kubwa sana hasa kwa vijana ambapo unakuta vijana wengi wanashindwa kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo yao, vijana wengi wamekuwa wanakariri kwa ajili ya kujibu mitihan. Kwa upande wangu bado naamini sana katika nguvu ya elimu, nikiangalia ugunduzi na maendeleo ya tecknolojia yanayoyokana na maendeleo ya elimu kwenye nchi zilizoendelea naamini bado Afrika na Tanzania tunaweza piga hatua kubwa sana kama tutaamua kwa dhati kuwekeza kwenye elimu ya watoto wetu hasa elimu ya vitendo yaani watoto tangu wakiwa watoto wasome kwa matendo wafanye tafiti mapema hii itasaidia watoto kukusanya uzoefu, kujifunza kwa muda mrefu na hatimaye kuanza kulitumia taifa mapema. Naipongeza serikali ya rais Magufuli kwa kutoa elimu bure ila nitaipongeza zaidi endapo tu serikali itawekeza zaidi kwenye elimu ya vitendo na tafiti.