Nakumbuka miaka mitano iliyopita kiwango cha elimu
Tanzania kilishuka kwa kiwango kikubwa sana. Baadhi ya vipengele katika elimu
vilibadilika kabisa na kusababisha elimu yetu kupoteza uhalisia wa elimu bora.
Katika elimu ya sekondari tuliona tulitoka kwenye division one hadi four,
tukaenda kwenye division 1 hadi E. Pamoja na Tanzania kujitahidi kuboresha
mifumo ya elimu kupitia Mpango wa maendeleo ya shule ya msingi (MMEM) na mpango
wa elimu wa shule za sekondari (MMES) hata baada ya kuwa madarasa mengi
yamejengwa na wanafunzi wengi kuandikishwa ila bado wananchi wamekuwa
wakilalamika kuwa elimu wanayopewa watoto ni ya hali ya chini kwam,ba watoto
hawajifuzi stadi muhimu watakaokuwa wanazitumia ili kupata kazi kuishi katika
jamii zao na kutoa mchango katika taifa .
Ubora wa elimu katika shule za msingi umekuwa mdogo
sana na kupelekea watanzania wengi tukiona bado madarasa
yaliyojaa kupindukia utoro mashuleni uhaba wa vitabu adhabu kali na vitisho
walimu wasio na sifa . Zaidi ya hapo wanafunzi huwa wanamaliza muda wote wa
masomo hawajajifunza stadi muhimu za maisha watazotakiwa kuzipata ili kubuni za
kazi kuishi katika jamii zao.
Changamoto yetu
katika nchi yetu ni kupata elimu bora ambayo kila mtu akimaliza shule ya kata ubora
wake uwe sawa na mtu aliyetoka katika shule za matajiri au shule za private. Katika kampeni ya mwaka jana tuliwasikia
viongozi wengi wakiahidi elimu bure na tumeona kweli hayo yametekelezwa lakini
tunahitaji kwa asilimia kubwa zaidi ya hapo. Pia wanafunzi wafundishwe kuhusu
stadi za maisha.