TUJIELIMISHE

Written by Angela Chizumi | Posted on  15 April, 2016.

Taifa lililoelimika ni taifa lenye mtazamo wa maendeleo, hii kauli inadhuhirishwa pia na baba wa taifa alipozungumzia maadui wakubwa wa Taifa, ikiwemo Ujinga, maradhi na umasikini na tuyatazama kwa umakini mambo haya yanategemeana kwa hali ya juu.

Taifa la watu wasiotafuta kujielimisha au kuelimika watakuwa wajinga na umasikini ukiwa kichocheo au kikwazo cha kuelimika tutazidi kuwa kwenye umasikini uliokithili, lakini zaidi tukakosa kutafuta tiba ya maradhi kwa hakika tutapoteza nguvu kazi ya taifa.

Ikiwa malengo ya Dunia yanahamasisha kuwepo na elimu bora na ikaweza kufanikiwa kwa asilimia 91% ilipofika 2015 kwa elimu ya msingi kupatikana kwa watu wote. Ingawa elimu kwa bara la Africa bado inajitahidi kuinuliwa.

Jambo la msigi hapa sio kufikia malengo ya maendeleo ya Dunia ila ni jinsi gani mtu anachukua jukumu la kuelimika kama la mtu binafsi, yaani kujielimisha. Hapa simaanishi uende kusome shada ya uzamivu wa uchumi au sayansi ya viumbe ila ni jinsigani kwa kila siku kwenye maisha yako unapotenga mda kidogo wakutafuta elimu, iwe kwenye vitabu, majarida, vipeperushi au kwa njia ya mtamndao.

Watanzania wengi inasemekana wanakosa maarifa kwa sababu tu hatupendi kusoma na  hii inaweza kuwa kweli, lakini ni jinsi gani tunatumia nafasi tulizonazo katika kijendeleza, namaanisha uliye shuleni unatumia vipi vitabu vya maktaba katika kusoma nakupata maarifa zaidi? Uliyekuwa ofisini unatumia vipi copyuta na internet yako katika kutafuta mawazo mapya? Ni jinsi gani tunatumia vitu tuivyonavyo kuongeza ujuzi wetu?. Ikiwa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 1977 inasisitiza kujielimisha kwenye ibara ya 11(2) “Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa juru kutafuta elimu katika fani anaypenda hadi kugikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake”. Ni kwa nini wananchi tusiamke nakuanza kusoma nakuitafuta elimu.